Friday, August 2, 2013

'Maadui zetu ndiyo wanasema Messi na Neymar hawatashirikiana' - Rais wa Barcelona

Sandro Rosell alludes to one more signing
Rais wa klabu ya Barcelona Sandro Rosell amesema kuwa mahusiano ya Messi na Neymar ndani na nje ya uwanja yatakuwa ni mazuri tofauti na watu wanavyosema. Rosell aliamua kuliongelea jambo hili mbele ya waandishi wa habari kwa uchungu akisema ni maneno ya chuki ya wapinzani wa Barcelona. ' Unajua wapinzani na maadui wa Barcelona wapo wengi sana, wanajaribu kutumia mwanya wa vyombo vya habari kuwafanya Messi na Neymar wawe maadui ili washindwe kushirikiana. Ujanja wao tunaujua na napenda kuwaambia kuwa Messi na Neymar ni marafiki tayari, vilevile kila mchezaji wa Barcelona anachokifikiria ni ushindi wa timu na sio kushindana mchezaji mmoja mmoja. Mwakani muda kama huu utafika na tutaona watasema maneno gani kwasababu maneno wanayosema sasa yatakuwa kinyume na watakachoshuhudia'. Rosell aliamua kuliongelea jambo hili kwasababu watu wengi wanaliongelea jambo hili kila mara, hali inayohisiwa linaweza kuwafanya wachezaji hawa wawe maadui, lakini kauli ya Rosell imelainisha joto lililokuwepo kuhusu jambo hili. Neymar anatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza pamoja na Messi leo kwenye uwanja wa Camp Nou baina ya Barcelona na Santos. 
Messi na Neymar wakiwa wamekumbatiana wiki hii kabla ya mechi ya kirafiki dhidi ya Lechia Gdansk kuanza nchini Poland. 
Messi na Neymar wakimsikiliza kocha leo asubuhi. 

No comments:

Post a Comment