Thursday, January 23, 2014

Rage amesema anahusika kumsimamisha Okwi

Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema yeye ndiye amehusika kusimamisha usajili wa mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga, Emmanuel Okwi. Rage ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wa watendaji wa klabu hiyo. Rage alisema aliamua kufanya hivyo kwasababu klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo Okwi aliuzwa akitokea Simba haikufuata utaratibu kama makubaliano yalivyosema kwenye mkataba. Kwa mujibu wa Rage, klabu ya Etoile du Saleh ilitakiwa kutoa asilimia kadhaa kwa klabu ya Simba wakati wa kumuuza mchezaji huyo kwenda timu yoyote, jambo ambalo halikufanyika. Sababu hii ndiyo imeifanya klabu ya Simba kuhusika kusimamisha usajili wa mchezaji huyu kupitia TFF na Okwi hatacheza mechi zozote za klabu ya Yanga hadi hapo TFF itakapotoa kibali. 

Wakati huo huo, uongozi wa klabu ya Simba umempandisha cheo  aliyekuwa afisa habari wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga na kuwa katibu mkuu mpya, Kamwaga anachukua nafasi ya Evodius Mtawala aliyepata ajira akiwa kama mkurugenzi wa kitengo cha wanachama na sheria TFF.
Ezekiel Kamwaga

No comments:

Post a Comment