Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa ulikuwa ni uamuzi mgumu kwake kumwachia Juan Mata kujiunga na wapinzani wao katika ligi kuu ya England Manchester United. Akizungumza na BBC Mourinho amesema " Haya ni maamuzi ambayo mkufunzi yoyote anapaswa kufanya, lakini kwangu ilikuwa vigumu. Nilipenda kuendelea kumuona Mata katika kikosi changu, Lakini kwa hali ilivyokuwa ililazimika aondoke na mimi nilipenda awe huru kwasababu napenda kuwaona wachezaji wangu wakiwa na raha. Ila nasikitika sikuweza kumfurahisha, nasikitika sana kwa hilo, lakini naendelea kujenga kikosi changu kwa kumfanya Oscar kucheza nafasi yake'
No comments:
Post a Comment