Leo saa tisa jioni kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Taifa Stars inashuka dimbani kupambana na Morocco katika mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Taifa Stars ipo nafasi ya pili na pointi 3, ikiweza kushinda mchezo wa leo itakuwa na pointi sita na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Morocco inafungika na uwezo wa kuifunga tunao, Stars ilionesha mchezo mzuri sana mwaka huu mwezi wa pili baada ya kuwafunga Cameroon goli moja katika uwanja wa taifa, nguvu na mbinu zile zile za kuwafunga Cameroon zinaweza kutumika kuwaliza Morocco. Tujitokeze kwa wingi katika uwanja wa taifa kuishangilia timu yetu ya Taifa. Mungu Ibariki Tanzania.
No comments:
Post a Comment