Tuesday, May 28, 2013

Kolo Toure ajiunga na Liverpool

Beki wa Man city Kolo Toure amesajiliwa na Liverpool bila ada yoyote baada ya mkataba wake na Man city kuisha. Toure anatarajiwa kujiunga rasmi na Liverpool tarehe 1 Juni na atakuwa ni raia wa kwanza kutoka Ivory Coast kuichezea Liverpool. Liverpool imefikia uamuzi wa kumsajili Toure ili kuziba pengo lililoachwa na Jamie Carragher aliyestaafu mwisho mwa msimu huu. Toure mwenye miaka 32 amecheza mechi 13 tu msimu huu akiwa na Man city na vilevile aliachwa kwenye kikosi kilichoshiriki michuano ya Uefa champions kutokana na upinzani mkali uliopo ndani ya klabu ya Man city kutoka kwa Kompany, Nastasic na Lescott hivyo imekuwa ni rahisi kwa Toure kufanya uamuzi wa kujiunga na Liverpool ili aweze kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment